Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ Kikosi cha 24KJ Mkoani Kigoma kimetakiwa kuendelea kukagua na kutembelea maeneo yao yote ya mapori yaliyopo Mkoani humo ambayo yamekuwa yakitumika na baadhi ya watu kufanyia vitendo vya uhalifu na ujambazi kuhakikisha yanatokomeza vitendo hivyo.
Hayo yamebainishwa wakati wa kuahirishwa kwa zoezi KIKAKA zoezi ambalo lililenga kuwajengea uwezo Askari na Maafisa wa Kijeshi katika uwanja wa vita juu ya matumizi ya silaha na maeneo yao katika Wilaya za Kasulu Kibondo na Kakonko.
“Kazi ya kuhakikisha ofisi zao ziko salama ni haki yao Askari wa Jeshi la Wananchi hivyo kuzijua ofisi zao na wanapaswa kuzilinda na kuhakikisha muda wote ziko salama , kwa kipindi chote cha mafunzo wameweza kujiimarisha vizuri zaidi na zoezi hilo ni endelevu nipende kuwahakikishia Wananchi kuwa eneo hilo ni salama na wafanye kazi kwa uhuru’’ Brigedia Mkunda.
POLEPOLE AMVAA “RC UNATAKA UBUNGE KIGAMBOMI, KUWA NA NIDHAMU KUFA NAYO”
https://youtu.be/BX0OnyARz9g