Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Benki ya CRDB uzidikuzingatia misingi ya utawala borana kuongeza juhudi katika utoaji wa huduma ili benki hiyo iendeleekuwa mfano wa mafanikio kwa taasisi zinazomilikiwa nakuendeshwa na wazalendo.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeendelea kuimarisha misingi ya utawala bora ili kuleta matokeochanya, hivyo ni vema kwa uongozi wa benki hiyo ukaizingatia.
“Serikali imeendelea kuhakikisha kwamba katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali kunakuwepo na uwazi, uwajibikaji, ushirikishaji wa watu, ufanisi, tija, uadilifu, usawa, kuzingatia taratibu za kisheria, kanuni na miongozo inayotolewa na Viongozi wakuu wa kitaifa.” Waziri MkuuWaziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kusisitiza misingi hiyo ya utawala bora ili kujiridhisha kuwa taasisi mbalimbali zikiwemo za kifedha zinaongozwa kwa kufuata misingi hiyo.
WALIOLIPUA MAWE YAKAHARIBU NYUMBA ‘TULIWAAMBIA TUTALIPUA ILA TUTAWALIPA‘