Taasisi ya Kuendeleza Kilimo Nyanda za juu Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) imesema Serikali ya Tanzania inatarajia kutiliana saini na Serikali ya Uholanzi, August 8 2018 kwa lengo la kuendeleza kilimo cha viazi mviringo nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya Nanenane mkoani Mbeya Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga amesema kupitia mkataba huu tija katika uzalishaji wa zao hili utaongezeka kutokana Teknolojia ya kisasa katika kilimo cha viazi.
“Mkataba huu utaleta makampuni ya kiholanzi yenye teknolojia mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa zao la viazi mviringo hivyo tija ya uzalishaji itaongezeka nchini,” amesema Kirenga na kuongezea kuwa lengo ni kuwainua wakulima kiuchumi na pia kujitosheleza kwa mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi