Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amewataka wananchi wa Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza mkoani Kigoma kuendelea kuwa watulivu na kuachana na tabia ya kushindana na serikali ambayo imekusudia kumaliza tatizo lililoibuka hivi karibuni Mkoani humo.
Waziri Mpina ameyasema hayo alipofika katika eneo ambalo hivi karibuni kulitokea vifo vya askari wawili pamoja na wananchi wawili wakati wa zoezi la kuwaondoa wananchi waliovamia eneo la Kampuni ya Ranchi za Taifa jirani na kijiji hicho.