Leo August 20, 2018 Basi la Kampuni ya Saratoga lenye namba za usajili T476 ADG lililokuwa likitoka mkoani Kigoma kwenda Sumbawanga limeteketea kwa moto eneo la Kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma.
Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Martin Ottieno limesema kuwa bado linachunguza chanzo cha moto huo.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, abiria wote wametoka salama na baadhi ya mizigo imeokolewa.