Vijana 7 wa umri wa miaka 21 hadi 24, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kosa la kuharibu Noti za Benki Kuu ya Tanzania (B.o.T) za Shilingi 70,000 kwa kuzikanyaga.
Washtakiwa hao ni Vicent Kaduma (Vice-24), Rogers Swale (23 ), Doreen Mwenisongole (22) ni mwanafunzi, Kelvin Mngeyekwa 23, Eia Chengula 24 mfanyabiashara, Said Sadiq 21 na Ramadhan Seleman 23.
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono chini ya kifungu cha 332 A cha kanuni ya adhabu.
Mbele ya Hakimu Mkazi, Wanjah Hamza wakili Kombakono amedai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kosa moja la kuharibu noti za B.o.T.
Inadaiwa washtakiwa walitenda kosa hilo, September 16,2018 wakiwa jijini Dar es Salaam ambapo pasipokuwa na mamlaka waliharibu noti za Shilingi 70,000 ambapo noti moja ikiwa na thamani ya Shilingi 10,000.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa walikana makosa ambapo Wakili Kombakono amedai upelelezi wa kesi haujakamilika.
Hata hivyo, washtakiwa hao walipatiwa masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini 2 waaminifu waliosaini bondi ya Shilingi Milioni 2 kwa kila nmoja. Kesi imeahirishwa hadi November 11,2018.
HUKUMU: Hawa hapa Wafanyakazi wa Benki waliohukumiwa miaka 28 jela