Mfanyabiashara Hamis Said (38), anayekabiliwa na kesi ya kumuua mkewe, Naomi Marijani ametoa vitisho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akidai atawafanyia kitu kibaya Waandishi wa Habari ambacho mahakama haijakitarajia.
Mfanyabiashara huyo ambaye yupo gerezani kwa siku 14 tangu alipofikishwa mahakamani hapo Julai 30, 2019 ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Salum Ally.
“Mheshimiwa nina kitu ambacho nataka nikueleze kuhusu Waandishi wa Habari wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya mahakama sasa nakueleza hivi nitakuja kuishangaza mahakama nitafanya kitu kibaya sana,”
Hata hivyo Wakili Wankyo amesema “Lengo la Waandishi wa Habari ni kutoa habari na kuwajuza wananchi, hivyo kumbuka hii ni mahakama na hatujui kitu unachotaka kufanya ni kitu gani,”
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 27, 2019 kwa ajili ya kutajwa
Mshitakiwa anakabiliwa na kosa la mauaji ambapo adaiwa alilitenda Mei 15, 2019 katika oneo la Geza Ulole Kigamboni Dar es Salaam ambapo alimuua mtu anayeitwa Naomi Marajani.
Inakumbukwa kuwa Hamis anadaiwa kumuua mke wake Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya Mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.