Sekta ya mawasiliano Tanzania ina wadau wakuu wanne ambao ni Serikali, Watoa huduma, Watumiaji wa huduma na TCRA ambaye ni msimamizi wa sekta. Wadau hawa wana majukumu, matarajio na malengo tofauti kama inavyoainishwa hapa chini: –
Serikali-inatunga sera, sheria na kanuni zinazoongoza sekta pamoja na kukusanya kodi
zinazotokana na shughuli za sekta kwa maendeleo ya nchi na watu wake.
Watoa huduma-wanafanya biashara, wamejipangavizuri, wanahamasishwa na kupata faida, wana
uwezo (nguvu ya fedha).
Watumiaji-hawajajipanga, wanatazamia kupata huduma bora kwa gharama kidogo au ikiwezekana
hata bure, hawana umoja na wengi wana ufahamu mdogo kuhusu teknolojia ya mawasiliano pamoja na huduma wanazozitumia.
Mdhibiti/Msimamizi (TCRA) – yuko katikati ya wadau hawa wengine ili kuhakikisha mahitaji na matazamio yao yanafikiwa kwa kuzingatia uwiano sawia wa manufaa katika sekta ya mawasiliano.
Mamlaka inatekeleza sera za Serikali, inahakikisha sekta haiyumbi kwa kuhakikisha watoa huduma
wanatoa huduma kwa ufanisi na kuona maslahi ya watumiaji yanalindwa.
TAZAMA MUONEKANO WA JUU WA MZUNGUKO WENYE SANAMU YA SAMAKI KIGOMA