Headline za sukari zimeendelea katika vyombo mbalimbali vya habari , Leo May 11 2016 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameendelea na zoezi la kuchunguza watu wanaodaiwa kuficha bidhaa hiyo ambapo ametembelea maeneo mawili tofauti na kubaini uwepo wa sukari inayosadikiwa kufichwa kwenye makontena.
Makonda amekuta makontena yenye sukari 115 ikisadikiwa kuwa ni mali ya Mohamed Interprises ambapo amaegiza vyombo vya usalama kuchunguza kwanini sukari hiyo haiko kwenye mzunguko wa biashara, pia kataka kujua ubora wa sukari hiyo kutokana na taarifa za awali kuonyesha imetengenezwa Brazil huku packaging ikifanyika Dubai.
Katika eneo lingine RC Makonda amekuta sukari zaidi ya tani 1300 ikidaiwa kuwa ni ya viwandani, Mkuu huyo wa mkoa ametoa saa 24 kupatiwa nyaraka zote pamoja na kuitaka Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA) kuhakiki ubora wa sukari hiyo.
Hapa ninazo picha 15 kukuonyesha namna ilivyokuwa katika msako huo…
ULIIKOSA HII DAR ES SALAAM NA WATUMISHI WAKE?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE