Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

DONE DEAL: Azam FC wameendelea kumuamini Donald Ngoma

on

Club ya Azam FC leo imefikia maamuzi mengine ya kuendelea kutambua mchango wa mshambuliaji wao wa kimataifa wa Zimbabwe Donaldo Ngoma anayechezea timu yao, kumuongezea mkataba mpya wa mwaka mmoja.

Azam FC walimsajili Donald Ngoma kama mchezaji huru baada ya kuachwa na club yake ya zamani ya Yanga kutokana na staa huyo kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwa madai ya kuuguza jeraha lake la kisigino kwa muda mrefu.

Wadau na mashabiki soka wengi waliipongeza Azam FC kwa kuchukua uamuzi wa kumsajili Donald Ngoma akiwa majeruhi na kuamua kumpeleka Afrika Kusini kumfanyia matibabu kwa gharama zao huku mchezaji akiwa hajaumia akiwa mikononi mwao, kitu ambacho ni nadra sana kwa vilabu kufanya.

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke 

Soma na hizi

Tupia Comments