Chuo Kikuu cha Kiislamu nchini Uganda kimewafukuza wanafunzi wake 23 kwa madai ya kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi jambo ambalo ni kinyume na kanuni za taasisi hiyo.
Mratibu wa chuo hicho, Dk. Sulait Kabali, ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Nidhamu, aliliambia gazeti la Daily Monitor kuwa wanafunzi hao wamefukuzwa kwa kuwa na mahusiano na kufanya mapenzi kwenye eneo la chuo.
Maamuzi hayo ya kuwafukuza wanafunzi hao yalifanywa na Kamati ya Nidhamu ya chuo hicho.
Watuhumiwa 24 wa Ugaidi wamekata rufaa mahakama kuu