Top Stories

Spika Ndugai “Zitto ni muongo, CAG nitamuonyesha Bosi wake” (+video)

on

Leo January 17, 2019 Spika wa Bunge Job Ndugai amesema Mbunge Zitto Kabwe anampa tabu sana kwa sababu yuko peke yake pale Bungeni na Chama chake kina Mbunge mmoja.

Ndugai amesema hayo leo alipoulizwa na Wanahabari kama atamchukulia hatua Zitto, “Yuko rafiki yetu mmoja aliwaita akawadanganya sijui kule Uganda aliitwa CAG wa kule sijui wakafanyaje, niliongea na Uongozi wa Bunge la Uganda wakaniambia that is big fat lie” Spika Ndugai

“Huyu Zitto Kabwe ni miongoni mwa Wabunge ambao wananisumbua sana kwa sababu amekuwa akipotosha mara kwa mara hebu nisaidieni Mtu kama huyu nimfanyaje” Spika Ndugai

“Si vizuri Kiongozi kudanganya Watu, kule Uganda na Kenya CAG ni Afisa wa Bunge, huyo Afisa wa Bunge anawezaje kumgomea Spika?, haelewi anachokiongea Zitto Kabwe, Mihimili ni mitatu huu wa nne umetoka wapi?” Spika Ndugai

“Ni kweli Zitto Kabwe ananisumbua sana lakini, ukisema umtoe Bungeni unawaza Mtu mwenyewe yuko peke yake ukimsimamisha atawakilishwa na nani? Unamuacha tu ndio maana hata kesi hizo anafanya peke yake maana yuko mwenyewe” Spika Ndugai

LIVE: Mkurugenzi TCRA anazungumza juu ya tukio la Rais Magufuli kesho

Soma na hizi

Tupia Comments