Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifunga kikao kazi cha Kamati ya Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto MTAKUWWA Mkoa wa Tabora ametangaza kuwachukulia hatua wanaume wanaonyanyasa wanawake huku akiapa kupambana na wazazi wanaochangia ongezeko la mimba na ndoa za utotoni.
“Usituletee hapa utamaduni wa ajabu ajabu unampiga Mkeo anakuja uso umefumuka huu ukatili mkubwa umetoa wapi haiwezekani tukaonekana wakatili, organizer nendeni muite akina mama wote wanaoonewa wanafanyiwa vurugu na waliotelekezewa watoto” RC Mwanri