Moto ambao chanzo chake hakijabainika katika Kata ya Sinoni Mkoani Arusha umeleta madhara kwa vyumba kumi na tatu baada ya vitu vilivyokuwa ndani kuungua nakusababisha watu kulala nje.
Kijana Hamid Hamis amedai moto ulipozuka walijitokeza watu wakaanza kuiba baadhi ya vitu pamoja na fedha zaidi ya Million 12 ambazo zilikuwa zimewekwa ndani kwa ajili ya kununulia kiwanja.