Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Hiki ndicho chakula ambacho Moyes aliwakataza kula wachezaji wa Man UTD

on

Manchester-United-v-Stoke-City-Premier-LeagueMiezi takribani 10 tangu atimuliwe kutoka kwenye nafasi ya ukocha wa klabu ya Manchester United, David Moyes ameelezea moja ya jambo lilokuwa linaisibu timu ya Manchester United wakati wa utawala wake na kutishia mafanikio ya timu uwanjani.

Akihojiwa na jarida maarufu la soka la FourFourTwo, David Moyes ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Real Sociedad ya Uhispania alisema tatizo kubwa lilokuwa linaisumbua timu lilikuwa ni wachezaji wengi kuwa na uzito uliopitiliza (Ubonge), kitu kilichopelekea aamue kuwapiga marufuku kabisa matumizi ya chips kwa wachezaji wake.

Ndio, ilibidi nipige marufuku chips“– Moyes.

Ilikuwa kwa sababu kulikuwa na wachezaji wengi ambao walikuwa na uzito uliopitiliza na sikudhani kama chips zilikuwa nzuri kwenye diet yao, hivyo nikapiga marufuku.”– Moyes.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments