Mix

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imeokoa hizi milioni ambazo zingetumika kwa matibabu nje

on

Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete kwa kushirikiana na hospitali ya BLK kutoka India kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo bila kuusimamisha moyo kwa kutumia mashine maalumu. Kaimu  mkurugenzi wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, Peter Kisenge amesema…..

>>>’matibabu haya tunatumia kama dakika 15 kwa kila mgonjwa na tumeshawafanyia wagonjwa kama nane, ni tiba ya aina yake kabisa tukishirikiana na wenzertu wa India, jana tu tumeokoa zaidi ya milioni 180 ambazo zingepeleka watu nje ya nchi wakati tungeweza kufanya hapa’.

Kwa mmujibu wa taarifa iliyotolewa inaeleza kwamba kwa siku mbili madaktari bingwa watatoa huduma kwa wagonjwa 18 na kwa siku ya kwanza wametoa huduma kwa wagonjwa 9. 

Taasisi kwa kuendelea kutoa huduma hii ya upasuaji mkubwa na kwa ubora zaidi, siku ya leo imesaini hati maalumu ya ushirikiano na taasisi ya India kwa ajili ya kuwapa mafunzo watumishi wake na kuendelea kutoa huduma ya upasuaji huu wa moyo kwa kushirikiana na taasisi hiyo ya BLK India.

ULIIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI ALIVYOENDA MUHIMBILI TENA NA KUKUTANA NA MENGINE? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPO CHINI

 

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments