Rais wa Sudan Omar al-Bashir ametangaza hali ya hatari nchini humo na kufutilia mbali utawala wa majimbo na uongozi wake.
Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, katika hotuba yake kwa Taifa Rais Bashir alisema kuwa maandamano yanayoshuhudiwa nchini yanalenga kuvuruga amani na kuhujumu utawala wake.
“Natangaza hali ya hatari kote nchini kwa mwaka mmoja. Natangaza kuvunjiliwa mbali kwa utawala wa majimbo katika ngazi zote hadi za mikoa.” Al-Bashir
Waandamanaji walimiminika katika Mji wa Omdurman baada ya tangazo hilo, lakini waliyoshuhudia wanasema maandamano hayo yalizimwa na polisi kwa kutumia mabomu ya machozi.
Saa kadhaa baada ya tangazo hilo rais Bashir amewateua Wakuu wa Vikosi vya Usalama kuchukua nafasi ya Magavana waliyofutwa kazi.
Katika hotuba yake kwa Taifa Bashir ameliomba bunge kuahirisha mchakato wa marekebisho ya katiba ambao ungemruhusu kugombe muhula mwingine madarakani.
Bashir pia alisema kuwa maandamano yanayoshuhudiwa nchini yanalenga kuvuruga amani na kuhujumu utawala wake.
RAIS MAGUFULI AFIKA KWA KIGWANGALLA, AMKUTA MKEWE AMPA POLE