Habari za Mastaa

EXCLUSIVE: Watoto waliowapiga chini Wema, Monalisa, Gabo kipengele cha Muigizaji Bora

on

Moja ya Story kubwa kwenye utoaji wa Tuzo za Sinema zetu ni pamoja na washindi wa kipengele cha mwigizaji bora wakiume na mwigizaji bora wakike ambao watu wengi walitegemea kuwaona mastaa kama Monalisa, Wema Sepetu au Gabo wakichua tuzo hizo kitu ambacho kilikuwa tofauti kwa usiku wa jana february 23, 2019.

Licha ya kwamba Gabo alishinda Tuzo mbili lakini hakuweza kufua dafu mbele ya kijana mdogo Rashidi Kasim ambaye ni chipukizi kwenye tasnia ya filamu aliyeibuka kidedea kwa kuchukua tuzo hiyo ya muigizaji bora wakiume huku tuzo ya muigizaji bora wakike akichukua Flora Kiyombo binti mdogo wa darasa la sita kitu kilichozua gumzo mtandaoni.

Bonyeza PLAY hapa chini kutazama watoto hao walioibuka washindi wakizungumza.

VIDEO: WEMA SEPETU KAFUNGUKA ‘NIMEJIKUTA NIKO NJE YA MUDA’

Soma na hizi

Tupia Comments