Habari za Mastaa

Matonya atoa ya moyoni baada ya WCB kutumia jina la wimbo wake ‘Zilipendwa’

on

Wasanii wa record labe la WCB wakiongozwa na Diamond Platnumz usiku wa jana August 25 2017 waliachia video mpya ya wimbo wao wa pamoja kwa mara ya kwanza, wimbo huo ambao unaitwa ‘Zilipendwa’ umefanana jina na wimbo wa zamani wa Matonya ‘Zilipendwa”

Wimbo umeimbwa na DiamondRayvanny, Harmonize, Rich Mavoko, Maromboso, Lavalava na Queen Darleen, muimbaji Matonya leo kupitia ukurasa wake wa instagram kaandika ya moyoni kutokana na wasanii hao kutumia jina la wimbo wake pasipo kushirikishwa.

“Nduguzangu wasafi / Nawapongeza sana kwa kazi mzuri mnazo zifanya / Nilifurahi Sana mlichokifanya kwa saida karoli dadaetu/ mlimuita mkamshirikisha akawapa Baraka zake/ kwangu mlishindwa nini?”

“Sina shida Ya Pesa nina shida Ya heshima cose najua dunia ni mapito/ kama mimi naibiwa haki yangu vipi wasanii wachanga? Basata mkowapi? Wadau Wa muziki mkowapi? Usipo ziba ufa tajenga kuta!! Khaaa tena Bila woga???? lakini haki itafata mkondo wake”

Tazama video zote mbili ya Matonya na WCB halafu naomba comment yako

HII NDIO VIDEO MPYA YA WCB AMBAYO INAITWA ZILIPENDWA

HII NI ZILIPENDWA YA MATONYA 

FID Q KAFUNGUKA: “Team KIBA hawajapenda, wanatukana… huwezi kunipangia” (+video)

Soma na hizi

Tupia Comments