Sara Duterte ambaye ni Mtoto wa Rais anayemaliza muda wake nchini Ufilipino Rodrigo Durtete atagombea Umakamu wa Rais wa Nchi hiyo kwenye Uchaguzi ujao wa mwaka 2022.
Baada ya miezi kadhaa ya fununu hizo hatimaye Tume ya Uchaguzi ya Nchi hiyo imethibitisha leo Jumamosi kwamba Sara atagombea nafasi hiyo kubwa nchini humo.
Rais Duterte aliwahi kunuliwa akisema kwasababu hana uwezo wa kuwania Awamu nyingine ya Urais, anataka kuwania Umaku wa Rais na kwa namna anavyoonekana angependa nafasi ya Urais iende kwa mmoja wa Watu wa familia yake na labda ikishindikana kwa Watu wake wa karibu sana, ili kuendelea kuwa salama na tuhuma mbalimbali zinazomkabili akiamini atalindwa na Rais ajaye.
Miongoni mwa waliotangaza kuwania Urais katika Uchaguzi ujao nchini humo ni Nyoman wa masumbwi kutoka nchini Ufilipino Manny Pacquiao.