Club ya Yanga leo ilikuwa katika uwanja wa Kambarage Shinyanga kucheza mchezo wake wa 20 wa Ligi Kuu dhidi ya Stand United, mchezo huo Yanga waliingia wakiwa na rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu msimu chini ya Kocha wao Mwinyi Zahera.
Yanga wakiwa na kikosi cha kamili wamekumbana na wakati mgumu baada ya kushindwa kupata matokeo na baada ya kujikuta wakiruhusu goli dakika ya 88 na nahodha wa Stand United Jacob Masawe akapiga mpira wa kichwa uliyotinga wavuni na kumshinda golikipa Kindoki.
Kipigo hicho sasa bado kinaifanya Yanga iendelee kuongoza Ligi ila wanabaki na point zao zile zile 53, wakati Stand United wamefikisha jumla ya point 25, Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 pamoja na kukosa mdhamini mkuu lakini imekuwa na changamoto kubwa.
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”