Michezo

Mukoko asaini mkataba wa miaka miwili TP Mazembe

on

Club ya Yanga imetangaza kuwa kiungo wao Tonombe Mukoko kutokea Congo DR anaondoka na kujiunga na TP Mazembe ya kwao Congo, Yanga hawajaweka wazi Mukoko kama kaenda kwa mkopo au kauzwa jumla ila taarifa zilizopo alikuwa na mkataba wa miezi sita na Yanga.

Awali Mukoko ilidaiwa kuwa aligoma kwenda TP Mazembe kwa mkopo na kuomba kuwa Yanga wachague kuvunja mkataba wake uliyokuwa umesalia wa miezi sita ila kwa mkopo hakutaka kwenda.

Saa chache zilizopita kupitia ukurasa wa TP Mazembe umeripoti kuwa Mukoko amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia TP Mazembe akiwa jijini Dar es Salaam na muda mchache ujao anaondoka kwenda Bahrain kujumuika na kikosi cha TP Mazembe kinachojiandaa na mchezo wa play off kufuzu Kombe la Dunia.

Soma na hizi

Tupia Comments