Top Stories

Mwanaume amuua mpenzi wake kwa kumuwekea sumu, kisha nae kujiua (video+)

on

Watu wawili wafariki dunia kwa kunywa sumu katika Kitongoji cha Mlandizi kata ya Mlandizi Tarafa ya Mlandizi Wilaya ya kipolisi Mlandizi Mkoani Pwani.

“Mnamo tarehe 5/9/2021 majira ya asubuhi huko katika Kitongoji cha Mlandizi Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni wapenzi walikutwa wamefariki katika makazi yao baada ya kunywa ya kitu kinachodhaniwa ni sumu, Watu hao ni Godfrey Pius Mandai (48) ambaye alikuwa ni Dereva wa Kampuni ya Yapi Merkez na veronica Gerald ( 42) Mfanyabiashara na mkazi wa Mtwara ambaye alisafiri kutoka Mtwara na kumfuata Mpenzi wake huyo Mlandizi.

“Mwanaume yule alitengengeza juisi ambayo ndani yake ilikuwa na sumu akampa Veronica akanywa na kufariki, Mwanaume alipoona Mpenzi wake amefariki na yeye akanywa na akafariki”- Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa .

“Chanzo ni wivu wa kimapenzi ambapo Mwanaume alikuwa anamtuhumu Veronica kuwa anafanya usaliti, kwenye eneo la tukio tumekuta chupa yenye masalia ya sumu na tumekuta pia karatasi ambayo inadhaniwa imeandikwa na mmoja wao na imeandikwa ‘HUU NI USALITI TU’-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa .

WANAJESHI WALIOMPINDUA RAIS CONDE, WAANZA KUWAPOKEA VIONGOZI MBALIMBALI

Tupia Comments