“Katika kipindi cha miezi 6, Serikali imeleta Mwanza shilingi Bilioni 344 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya wananchi ikiwemo Bilioni 219.1 ya kutekeleza miradi ya ujenzi ambapo Bilioni 44.7 zitatumika katika ujenzi wa Stendi ya Nyamhongolo na Nyegezi”
“Serikali imeleta shilingi Bilioni 18 kwa ajili ya ujenzi wa MV Mwanza yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo, kazi imefikia asilimia 89, Ujenzi wa meli unatarajiwa kukamilika Mei, 2022 kwa gharama ya shilingi Bilioni 89.154, Serikali imeleta Mwanza Bilioni 15.2, Bilioni 8.3 kwa ajili ya kujenga Hospitali 3 za Wilaya, kumalizia Hospitali 2 za Wilaya, kujenga Vituo vya Afya 5 na Zahanati 21,kukarabati na kujenga vituo vya huduma 48 pia zimeletwa Bilioni 6.4 za kununulia dawa”
“Serikali imeleta shilingi Bilioni 174 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Kigongo – Busisi lenye urefu wa kilometa 3.2 pamoja na barabara za kuingia darajani zenye urefu wa kilometa 1.66, mradi huu hadi ukikamilika utagharimu shilingi Bilioni 699.278”
“Serikali inaendelea na dhamira yake ya kuliimarisha Jiji la Mwanza ambapo tayari imeshafanya mazungumzo na mwekezaji atajayejenga hotel ya kuelea majini katika Ziwa Victoria itakayosaidia kuvutia watalii na kupendezesha Jiji”——— Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akiwa Mwanza leo