“Takwimu za mpaka Oktoba 15, 2021 zinaonesha Watanzania 940,507 wamepokea chanjo ya UVIKO -19 sawa na 88.9% ya chanjo zote 1,058,400 aina ya JJ, shehena ya chanjo 1,065,000 aina ya Sinopharm zilizokuja kutoka China zimeanza kusambazwa katika Halmashauri na Mikoa yote”
“Tunatarajia kupokea chanjo aina ya Pfizer dozi 500,000 mwishoni mwa mwezi Oktoba kutoka COVAX FACILITY ambazo ni sehemu ya Dozi Milioni 3.7 za chanjo aina ya Pfizer ambazo nchi yetu itazipata kwa awamu kutoka COVAX FACILITY, tayari majokofu ya baridi kali 14 yenye uwezo wa kuhifadhi chanjo zote Milioni 3.7 yameshafungwa pale Jijini Dar es Salaam”
“Napenda kuwajulisha kuwa fedha zilizotolewa na IMF Shilingi Trilioni 1.3, Wizara ya Fedha na Mipango tayari imekamilisha maandalizi ya kugawa fedha hizo kwenda kwenye miradi husika ikiwemo ya kujenga madarasa 15,000, kununua madawati 462,795 ”
“Miradi mingine ni kujenga shule shikizi 3,000, kumalizia vyuo vya VETA 32, kununua magari ya wagonjwa 395, kununua vitanda vya hospitali 2,700, kununua xray mashine 85, CT Scan 29, mitungi ya gesi 4,640, kujenga ICU 72 na kununua mitambo 5 ya kuchimba visima vya maji”——— Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akiwa Mwanza leo