Kamanda wa Polisi Morogoro Wilbrod Mutafungwa ametoa onyo kwa Askari wa Usalama Barabarani kuacha vitendo vya kukagua nyaraka za Madereva ofisini badala yake ukaguzi huo ufanyike ndani ya magari ili kuepusha rushwa.
“Huu utaratibu mlionao wa kupeleka nyaraka kule chumbani kuanzia leo hii marufuku, ukaguzi unafanyika kwenye gari, kama Askari hawezi kukufata kwenye gari wewe subiri usiondoke nipigie simu nitakuja kukuondoa mimi mwenyewe, hatuhitaji utendaji kazi wa gizagiza huu ndio unaleta rushwa” RPC Morogoro
Kamanda Mutafungwa ametoa onyo hilo alipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika stendi ya mabasi ya Msamvu Morogoro.
MAUAJI YA MWANACHUO WA KAMPALA: MAMBOSASA ATOA MAAGIZO “LAZIMA TUTAJIBU”