May 16 2016 Bunge la 11 limeendelea Dodoma, ilikuwa ni nafasi kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwasilisha hotuba yake ya makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Lakini ilipofika wakati wa Kambi ya upinzania Bungeni kuwasilisha hotuba yao, ikazuiliwa kusomwa baada ya Mwenyekiti wa Bunge Mussa Zungu kuwataka kuondolewa kwanza kwa baaadhi ya maneno yaliyodaiwa kuwa yamekiuka kanuni na taratibu za Bunge
Nje ya Bunge Mbunge wa Arusha Godbless Lema na Easter Bulaya wanazungumza na Waandishi wa habari ‘Mikataba yote inapita kwa Mwanasheria wa Serikali, kamati ndogo imeondoka hapa bila kumuhoji Mwanasheria. Je, mkataba ule ulikuwa ni tata au sio tata?‘ –Godbless Lema
Kuna taarifa za ndani kuna vita inaendelea ndani ya biashara ndani ya mambo haya, hawataki taarifa za Lugumi ziongelewe, mimi kwenye hotuba yangu aliyekuwa IGP Mwema, Emmanuel Nchimbi wote waondolewe, waitwe na wakamatwe.’ –Godbless Lema
Unaweza kuwasikiliza wote kwenye hii video hapa chini…
ULIIKOSA HII WIZARA YA MAMBO YA NDANI IMELIOMBA BUNGE KUPITISHA BAJETI YAKE YA BILIONI 864?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE