Aliyekua Mbunge wa Mbinga Maharibi Kapten John Komba leo amepumzishwa kwenye makazi yake ya milele na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya Watanzania kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania ambao walikusanyika kwa ajili ya kumsindikiza kwenye safari yake ya mwisho.
Ibada ya sala imeongozwa na Askofu wa Jimbo kuu la Mbinga Askofu John Ndimbo na kuhudhiriwa na Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete,Spika wa bunge la Tanzania Anna Makinda,wabunge mbalimbali,viongozi wa dini pamoja na wananchi.
Kapteni John Komba amezikwa leo March 03 kwenye makaburi ya Mission yaliyopo Kijijini kwao Lituhi ambapo mazishi hayo yalitanguliwa na ibada iliyoanza saa 5 asubuhi na mazishi yalikamilika saa 10 jioni,Rest in peace Kapten John Komba.