Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana leo natumia muda wangu kukusogezea na haya yaliyoandikwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ukurasa wake wa Twitter kuhusu mauaji ya albino, vitambuisho vya taifa na kifo cha marehemu Kapteni John Komba.
Nafarijika na ushiriki mzuri wa wananchi katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura toka lilipoanza mwezi Februari huko Makambako.
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Tujitokeze kwenda kujiandikisha katika maeneo yetu kama itakavyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Tuitumie fursa hii wakati huu muafaka. — Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Watakaojiandikisha wakati huu ndio watakaopiga kura ya maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu. (1)
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Vitambulisho vya zamani vya mpiga kura havitatumika. Wote ambao ni Watanzania & wana umri wa miaka 18 au zaidi lazima kuandikishwa upya. (2) — Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Wanasiasa, dini na asasi za kiraia tuungane na Serikali na Tume ya Uchaguzi katika kuwakumbusha na kuwahamasisha wananchi wakajiandikishe.
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Kupiga kura kuamua kuhusu Katiba Inayopendekezwa au kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani ni haki na wajibu wa kila raia. (1) — Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Lakini, kuipata haki hiyo na kuweza kutimiza wajibu huo kunategemea kuwa na kitambulisho cha mpiga kura. Bila ya hivyo haiwezekani. (2)
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Kabla ya kura ya maoni juu ya Katiba Inayopendekezwa tumesisitiza wananchi kuisoma na kuielewa. Vitabu 1,558,805 tayari vimechapishwa. (1) — Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Nakala 1,341,300 zimesambazwa. Nakala 1,141,300 zimesambazwa kwenye mikoa 25 Tanzania Bara na nakala 200,000 zimegawiwa kwa Zanzibar. (2)
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Kwa upande wa Tanzania Bara kila Kata imepewa vitabu 300, ikiwa na maana ya vitabu 60 kwa kila kijiji. (3) — Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Tume ya Uchaguzi itatoa maelekezo ya elimu kwa umma. Asasi za kiraia 420 (Bara) & 75 (Zanzibar) zimejiandikisha kwa ajili ya zoezi hilo. (4)
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Tume ya Uchaguzi pia itatoa maelekezo husika kuhusu kampeni ya Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekwa wakati ukiwadia. (5) — Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Mauaji ya albino ni jambo linalofedhehesha na kulidhalilisha taifa letu. Wakati wote Serikali imelipa uzito mkubwa suala hili. (1)
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Naungana na Chama cha Albino Tanzania kulaani ukatili huu na kutaka hatua madhubuti zichukuliwe dhidi ya wahusika. (2) — Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Tumeshughulikia wahalifu hawa na tumefanya hivyo bila ya kuchoka tangu tukio la kwanza baada ya mimi kuingia madarakani Aprili 17, 2006. (3)
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Mwaka 2006 mpaka 2015, watuhumiwa 139 wametiwa nguvuni, miongoni mwao wako watuhumiwa 16 wa matukio ya Desemba na Januari mwaka huu. (4) — Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Mashauri 35 yamefunguliwa mahakamani na kati ya hayo 10 bado yanaendelea na yapo katika hatua mbalimbali. (5)
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Watuhumiwa wamepatikana na hatia. Kati ya hao waliopatikana na hatia 13 wamehukumiwa kifo na wawili wamepata kifungo cha miezi 6. (6) — Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Hatuwezi kushinda uhalifu bila ushirikiano baina ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama. Tuendelee kuwafichua wahusika. (7)
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Februari 28, 2015 tulipata habari ya majonzi makubwa ya kifo cha Mbunge wa Mbinga Magharibi, Mheshimiwa Capt. John Damian Komba. (1) — Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Kifo chake kimeliondolea taifa letu mmoja wa viongozi wazuri, msanii mahiri, raia mwema na mzalendo wa kweli. (2)
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015
Alitumia muda mwingi na vipaji vyake kuitumikia nchi yetu katika mambo mbalimbali. Tuungane na familia yake kumwombea mapumziko mema. (3) — Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 3, 2015