Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Rapper Future akataa kuhusishwa na ishu ya bodyguard wake kupigwa

on

Siku ya jana July 22,2019 stori kubwa ambayo ilitrend kwenye mitandao ya kijamii ni video fupi ambayo ilimuonyesha bodyguard wa Rapper Future akivamiwa na kupigwa vibaya mjini Ibiza Hispania huku chanzo cha kuvamiwa kinadaiwa kuwa ni ubaguzi wa rangi.

Inaelezwa kuwa Future alitua uwanja wa ndege nchini humo na watu 10 walimfuata na kuomba kupiga nae picha lakini aliwakatalia na ndipo hapo walipomtolea maneno yanayosemekana ni ya kibaguzi lakini ukiangalia vizuri video hiyo Future ameonekana kuwepo maeneo hayo lakini alionekana kutoingilia ugomvi huo wala kumsaidia bodyguard.

Sasa mashabiki wamemjia juu Future na kumtolea lawama kibao, hivyo Future aliamua kuzama kwenye insta story yake na kusema kuwa video hiyo ime-editiwa wamemfanyia figisu na kudai kuwa hakuwepo eneo la tukio na hajui kilichotokea na ameomba mashabiki wasimuhusishe kwenye jambo hilo tena.

VIDEO: UKIMUULIZA AIKA KUHUSU NDOA YAKE NA NAHREEL ATAKUJIBU HIVI

Soma na hizi

Tupia Comments