Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Mahakama yamkuta na hatia Katy Perry baada ya kuiba wimbo

on

Kwa mujibu wa mtandao wa The NewYork Times umeripoti kuwa mwimbaji Katy Perry amekutwa na hatia kutokana na kesi iliyokuwa ikimuandama juu ya hatimiliki ya ngoma ‘Dark Horse’ ambayo ilidaiwa kuwa iliigwa.

Inaripotiwa kuwa Jumatatu ya July 29,2019 Mahakama mjini New York imethibitisha kuwa wimbo huo wa ‘Dark Horse’ uliotoka rasmi mwaka 2013 ni copyright kutoka kwenye wimbo wa ‘Joyful Noise’ ulioimbwa na mwimbaji wa Gospel Flame ambaye jina lake halisi ni Marcus Gray, imeelezwa kuwa producer wa Katty Perry, Dr Luke alikiri mbele ya Mahakama kuwa hakuwahi kusikia wimbo wa Joyful uliotoka mwaka 2009.

Katty Perry alisema kuwa anaweza kuimba wimbo wake ‘Live’ mbele ya Mahakama lakini ilishindikana kutokana na wakili wake kupata hitlafu ya vifaa na kushindwa kucheza ngoma ya ‘Dark Horse’, hata hivyo mmoja wa Wakili wa Flame alisema kuwa Perry aliwahi kuwa muimbaji wa Injili kabla ya kuingia kwenye ngoma za kawaida.

Imeripotiwa kuwa Mahakama imewakuta na hatia watu sita akiwemo muandaaji wa nyimbo (prouducer), mtunzi wa nyimbo Sarah Hudson na Juicy J na kuelezwa kuwa itawekwa wazi kiasi atakachotakiwa kulipa Katy Perry kwa Marcus Gray.

VIDEO: ‘WATARAJIE NDOA, NISHAMTAMBULISHA TUNDA KWA WAZAZI ” WHOZU

Soma na hizi

Tupia Comments