Michezo

Jose Mourinho kamtolea uvivu Paul Scholes “rudi tena studio”

on

Baada ya mchezaji wa zamani wa Man United amabaye alikuwa kocha wa Oldham FC ya Ligi ya Pili nchini England Paul Scholes kujiuzulu katika club hiyo kwa kudumu kwa siku 31, kocha Jose Mourinho amemkosoa kwa kejeli na kueleza kuwa ukocha sio kazi ya kuongea.

Jose Mourinho ametoa kauli ya kumkosoa Scholes baada ya kudumu na timu hiyo kwa siku 31, huku akimwambia hivyo kachemka kwenye ukocha arudi tena studio akaendelea na kazi ya uchambuzi wa soka kama ambavyo alikuwa anafanya katika kituo cha Sky Sports.

“Paul Scholes alikuwa akinikosoa mimi nilipokuwa kocha katika vilabu mbalimbali vikubwa duniani wakati yeye ameweza kuifundisha club kwa siku 31 tu akiwa na Oldham Athletic, arudi tena studio”>>>Jose Mourinho

Sababu kubwa iliyompelekea Scholes kujiuzulu nafasi yake hiyo ni kutokana na tuhuma za kuingiliwa majukumu na mmiliki wa club hiyo, kitu ambacho hakukipenda na kuamua kubwaga manyanga akiwa ana siku 31 tu katika nafasi ya ukocha wa Oldham inayoshiriki League Two nchini England.

Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!

Soma na hizi

Tupia Comments