Ndege ya kijeshi iliokuwa na abiria 38 imetoweka ikielekea Antarctica, kulingana na taarifa ya Jeshi la wanaanga wa Chile ndege hiyo ya kijeshi ya Chile imetoweka na abiria 38.
Ndege hiyo kwa jina C-130 Hercules ilitoweka majira ya saa kumi na mbili muda wa Chile baada ya kupaa kutoka Mji wa Kusini wa Punta Arenas.
Miongoni mwa waliotoweka na ndege hiyo ni wafanyakazi 17 na abiria 21 ambao walikuwa wakisafiri ili kutoa usaidizi wa kimipango.
Wanaanga wa Chile wamesema kwamba operesheni ya usakaji na uokoaji inaendelea ili kuiokoa ndege hiyo pamoja na abiria wake.
Kitengo cha habari cha EFE kimeripoti kwamba watatu kati ya abiria hao ni raia.
Rais wa Chile Sebastian Pinera amesema katika ujumbe wa Twitter kwamba amefadhaishwa na kutoweka kwa ndege hiyo na kwamba anachunguza hali katika kambi ya wanahewa ya Cerrillos katika mji mkuu wa Santiago.
RC MWANRI ATAMANI KUTUMIA HELIKOPTA KWENYE KILIMO “TUTAZALISHA TANI 15,000”