Michezo

Hii ndio ndege ya mashabiki wa Manchester United watakayopaa nayo kesho kumpinga Moyes?

on

Screen Shot 2014-03-28 at 9.34.15 PMNilikua nacheki shaffihdauda.com ambayo ni website inayotoa stori za michezo ya ndani na  nje ya bongo ambapo imetoa hii ripoti na picha kuhusu mashabiki wa Manchester United wanaochukizwa na mwenendo wa timu yao chini ya uongozi wa David Moyes wamefanikiwa kupata ndege itakayopita juu ya paa la uwanja wa Old Trafford jumamosi ya kesho huku ndege hiyo ikiwa imebeba bango la ‘Moyes Out’.

Ndege hiyo imepangwa kupita juu ya paa la OT kwa dakika 10 kabla ya mchezo kuanza na baadae kwa dakika 5 na wakati wa mchezo vs Aston Villa.
Kundi la mashabiki hao tayari limethibitisha kwamba kesho ndege hiyo yenye bango la  “Wrong One: Moyes Out.” itafanya kama walivyopanga.
Bango hilo ni kinyume ya lile walilotaka kulishusha kutoka kwenye jukwaa la Stretford End linalosomeka  ‘Chosen One’.
Screen Shot 2014-03-28 at 9.58.52 PM

Tupia Comments