Habari za Mastaa

Nelly aomba radhi kwa video chafu kuvuja

on

Mwanamuziki nguli kutoka nchini Marekani Cornell Iral Hynes Jr maarufu kwa jina la kisanii Nelly, amejitokeza kuomba radhi kufuatia kitendo cha kurusha kipande kidogo cha video kilichohusisha maudhui yasiyofaa, yanayomuonesha mwanamke akifanya vitendo vya faragha

Video hiyo aliichapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (Insta story)

Nelly amesema video hiyo ni ya zamani na haikukusudiwa kuwekwa kwenye ukurasa wake huo wenye jumla ya wafuasi zaidi ya milioni 3 na kwamba hajui ni nani aliyeiweka.

Sakata la rapa huyo lilianza kuvuma zaidi siku ya jumanne kwenye mtandao wa Twitter baada ya kundi kubwa la watu kuona kipande hicho cha video kisichofaa kwa hadhira. ambacho kilifutwa muda mfupi tu baada ya kuchapishwa

“Ninaomba msamaha wa dhati kwa mwanadada huyo na familia yake, jambo lilitokea si la kufaa.

Hii ilikuwa video ya zamani ambayo ilikuwa ya faragha na haikukusudiwa kuwekwa hadharani.” Alisema Nelly alipozungumza na TMZ.

Soma na hizi

Tupia Comments