Afisa Mifugo na Uvuvi wa Wilaya hiyo Aldo Mwapinga ametoa taarifa ya katazo hili kutokana na vifo vya nguruwe 21 Wilayani humo na amenukuliwa akisema “Kata ya Tandala kumeripotiwa dalili za ugonjwa wa homa ya Nguruwe kwahiyo tunaendelea na jitihada za kuhakikisha tunashirikiana na Watendaji kuanzia ngazi ya Kata hadi Vitongoji kutoa taarifa juu ya hali inavyoendelea”
Amesema Serikali imepiga marufuku hiyo hususani katika kata ya Tandala huku pia akizuia utoaji wa Nguruwe kutoka kwenye zizi moja kwenda jingine kwa ajili ya kupandisha kwa jike, vilevile amewataka Watu kuacha kufukua Nguruwe waliofukiwa baada ya kufa (mizoga) na kuwachinja kisha kwenda kuuza nyama hizo vilabuni nyakati za usiku, hii ni baada ya taarifa za namna hiyo kuripotiwa hivi karibuni.