Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa kesi inayomkabili Rapper Asap Rocky ambaye kwa sasa yupo rumande nchini Sweden imeanzwa kusikilizwa leo July 30,2019 katika Mahakama ya mji wa Stockholm ambapo Rapper huyo amekanusha mashtaka dhidi yake.
Imeelezwa kuwa Wakili wa Asap Rocky aliielezea Mahakama kuwa mteja wake hakusababisha majeraha kwa makusudi bali alifanya hivyo kwa nia ya kujihami baada ya kijana huyo aliyetambulika kwa jina la Mustafa Jafari ambaye ndio mshataki kutaka kumfanyia vurugu.
Imezidi kuripotiwa kuwa shahidi ambaye alitakiwa kutoa taarifa mbele ya Mahakama kuhusu kesi inayomuandama ASAP Rocky amekamatwa kwa kesi ya wizi na ukabaji huku Mustafa Jafari ambaye anadai kushambuliwa na ASAP aliwahi kushtakiwa kwa kosa la kumpiga mtu kwenye mtaa wa Stockholm mwaka 2016.
Asap Rocky alishikiliwa na polisi nchini Sweden tokea July 30,2019 kwa tuhuma za kumpiga shabiki mmoja kwenye mitaa ya Stockholm huku sababu kubwa ya ugomvi huo ukitajwa kuwa ni headphones za Asap ambazo zilidaiwa kuharibiwa.
VIDEO: ‘Watarajie ndoa, nishamtambulisha Tunda kwa Wazazi” -Whozu
rrrrrrrr