Club ya Man United inawezekana kwa kiasi kikubwa imezima ndoto za Liverpool kutaka kutwaa taji la Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya miaka 29, hiyo ni baada ya Man United kuruhusu kupoteza mchezo kwa magoli 2-0 dhidi ya wapinzani wakuu wa Liverpool club ya Man City katika mbio za Ubingwa.
Kimsingi Man United angefanikiwa kuzuia Man City kuondoka na point zote tatu Old Trafford Liverpool wangekuwa wananafasi ya kuishusha Man City katika king’anyiro cha Ubingwa kwani timu zote hizo zimepishana point moja Man City akiongoza kwa point, magoli ya Benardo Silva dakika ya 54 na Leroy Sane dakika ya 65 ndio yalitoa uhakika wa Man City kuondoka Old Trafford na point 3.
Ligi ya msimu huu inaonekana hadi game ya mwisho ndio itaamua Bingwa nani, kwani kila timu kati ya Liverpool na Man City zinazowania Ubingwa huo, zimebakiza michezo mitatu, rekodi inamtetea Ole Gunnar Solskjaer ambaye wanadai kuwa toka apewe mkataba timu hiyo haifanyi vizuri tena kama alivyokuwa kocha wa muda.
Ukweli Solskjaer kapita kwenye nyayo za makocha wenzake waliopita Man United David Moyes, Louis van Gaal na Mourinho ambao wote wakikutana na Man City kwa mara ya kwanza wakiwa makocha wakuu wa timu hiyo walipoteza michezo.
Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23