Ni June 19, 2023 ambapo kumefanyika mjadala wa kitaifa ambapo ulihudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Ubunge Prof Kitila Mkumbo, Mfanyabiashara Rostam Aziz, Jenerali Ulimwengu pamoja na wadau mbalimbali.
Mjadala huo uliowakutanisha watu wao katika ukumbi wa Serena Hoteli Jijini Dar es Salaam, Mada kuu ni kulinda kuendeleza Umoja wa kitaifa wakati wa Mageuzi ya kisiasa na Kiuchumi.
Hizi ni nukuu za Mfanyabiashara kwa alichokuwa akikizungumza katika Mjadala huo.
‘Tumeishi katika vijiji mbalimbali, watu wa dini mbalimbali. Mpaka leo nchi yetu tunaishi hivyo bila kubaguana haya mambo si ya bahati mbaya taifa letu linapaswa kujivunia, Wenzetu wapo kwenye ubaguzi mpaka leo’- Mfanyabiashara Rostam Aziz
“Nchi yetu ina bahati sana. Ni kisiwa cha amani katika eneo lenye migogoro mingi. Lazima tuwashukuru waasisi wetu ambao wametubeba mpaka leo tupo salama salmini. Leo hii mtu haulizwi ni dini gani wala kabila gani”-Mfanyabiashara Rostam Aziz
“Leo hii tunaposema mtu kwa sababu ni mzanzibar ndio maana amefanya maamuzi haya, kesho tusiseme huyu Rais Ametoka Mbeya hana haki ya kufanya maamuzi kuhusu Mngoni wa Mara. Maanake mkianza hilo jambo haliishi.”– Rostam Aziz
“Naunga mkono mijadala. Lakini kwenye hili mjadala wa kiuchumi, mjadala wa kibiashara umegeuzwa kuwa mjadala wa kisiasa, kidini na ukabila. Mjadala umekua na ushabiki zaidi badala ya kutaka kujua ishu ni nini.”- Rostam Aziz