Duniani

Sheria ya kunyoa nywele Korea Kaskazini ambayo haipatikani kwingine duniani

on

Kila sehemu kuna taratibu zake ambazo lazima zifuatwe na watu wa sehemu husika huku taratibu hizo zikisimamiwa na kulindwa ambapo kwenda kinyume chake huweza kupelekea aliyeacha kuzifuata kuadhibiwa.

Leo May 1, 2017 ninayo hii stori inayomuhusu kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kuwaambiwa watu wa nchi hiyo kwamba kuna mitindo 28 tu ya nywele ambayo watu wanaruhusiwa kuchagua wanapotaka kunyoa.

Katika mitindo hiyo, wanaume wanaweza kuchagua mtindo mmoja wa kunyoa katika mitindo 10 iliyokuwa maalum kwa ajili yao, wakati mwanamke atachagua mtindo mmoja wa nywele kati ya 18 iliyowekwa kwa ajili yao.

Mbali na list hiyo, hakuna mtu anayeruhusiwa kunyoa kama kiongozi – yaani mtindo wa nywele wa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un haupo kwenye list ya mitindo 28, hivyo hakuna anayeruhusiwa kunyoa kama yeye.

Watu wazima wanaruhusiwa kukuza nywele hadi kufikia urefu wa inchi tatu, lakini watu wengine wameonywa kutozidisha nywele zao zaidi ya inchi mbili huku wanawake walioolewa wakiambiwa wafupishe nywele zao.

Miongoni mwa mitindo iliyopigwa marufuku nchini humo ni pamoja na Spiky crops na uvunjaji wa kanuni hii kunaweza kukufanya kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Mitindo 10 kwa wanaume:

Mitindo 18 kwa wanawake:

VIDEO: Ilivyokuwa kwenye Harusi ya Madam Flora, Mwanza. Bonyeza play kutazama…

Soma na hizi

Tupia Comments