Moja ya habari kubwa za wiki hii ni huu uamuzi wa Marekani kutangaza kwamba itaanza kuwaruhusu Abiria wa kimataifa waliochanjwa chanjo kamili ya COVID-19 tu.
Naibu Afisa wa Habari katika Ikuku ya White House Kevin Munoz ametangaza hilo kupitia ukurasa wa Twitter na kuongeza kuwa sera hiyo itaongozwa na uzingatiaji wa afya ya umma na masharti yaliyopo mara kwa mara.
March 2021 mwaka uliopita Marekani ilifunga mipaka na kuwazuia Wasafiri kutoka mataifa mengine ikiwemo Umoja wa Ulaya, China, Uingereza, India na Brazil kama juhudi za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona na sasa chini ya sera mpya iliyoainishwa mwezi uliopita Wasafiri ambao wamepata chanjo watahitaji kupimwa kama kawaida siku tatu kabla ya kusafiri kwenda Marekani.