Leo June 17,2019 mwimbaji kutokea kwenye industry ya Bongo Fleva Alikiba amekutana na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Frederick Clavier na wamezungumza namna ya kuweza kujenga daraja la kukuza utamaduni uliopo kati ya Tanzania na Ufaransa.
Hii ni hatua kubwa kwa Muziki wa kizazi kipya na sekta ya burudani kwa ujumla kutokana na juhudi ambazo zinaonyeshwa na wasanii kwa kuipeperusha vyema bendera ya Taifa pamoja na lugha ya Kiswahili inayotumika mara nyingi katika kutunga nyimbo zao.
“Mapema asubuhi ya leo nilipata fursa ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini – His excellence Frederic Clavier ofisini kwake. Tumezungumza mengi kuhusu namna gani tunaweza kujenga daraja la kubadilishana utamaduni baina ya Tanzania na Ufaransa.” >>>aliandika Alikiba
AUDIO: ULIPITWA NA HII YA WEMA SEPETU KUPELEKWA GEREZANI SIKU 7? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUFAHAMU MWANZO MWISHO