Magazeti

CCM na Urais 2015.. Gwajima alitaka kutoroshwa? Askofu Pengo kasemaje? Sikiliza hapa

on

volume-button-19751-1680x1050

Jumatatu  ya March 30, tayari  Magazeti ya leo yapo mtaani, POWERBREAKFAST ya CLOUDS FM nayo imeshafanya uchambuzi wa stori zote, kama zilikupita sikiliza hapa…

Iko ishu ya Urais CCM kuwa na dalili za maamuzi magumu, Muswada wa Sheria ya makosa ya mtandao unaelekeza atakayesambaza picha cha ngono mtandaoni kufungwa miaka 7, Askofu Kardinali Pengo amesema amemsamehe Askofu Gwajima kwa kumkashifu, Jeshi la Polisi Dar linawashikilia watu 15 kwa tuhuma za kutaka kumtorosha Askofu Gwajima katika Hospitali ya TMJ, Askari Magereza afukuzwa kazi kwa kosa la kukutwa na fedha bandia, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesitisha kuanza kwa mradi mpya wa mji wa Kigamboni.

Zitto Kabwe kapewa masharti magumu na chama cha ACT, barabara ya msimbazi kufungwa ili kupisha ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi, Wizara ya Uchukuzi inatarajia kujenga reli mpya tatu ili kutoa huduma kwa nchi jirani na Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ametoa wito kwa vijana wa Afrika kupinga ukoloni mamboleo.

Katika uchambuzi huo kulikuwa na mazungumzo ya Askofu Kardinali Pengo ambae amesema amewasamehe wale wote walioeneza hivi karibuni maneno ya kashfa yasiyofaa dhidi yake.

92.9 Clouds FM inasikika ukiwa Iringa.

Bonyeza play kusikiliza uchambuzi wote wa Magazeti ya leo March 30.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments