Mijadala imezuka kwenye mitandao ya kijamii baada ya vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa kuonesha video inayomwonesha tembo anatokwa na moshi mkubwa mdomoni mwake.
Wanasayansi wa wanyamapori pia wameonesha kushangazwa na kitendo hicho. Kutoka nchini India video hiyo ilionesha tembo huyo akiokota mikaa wa moto msituni kwa kutumia mkonga wake na kuingiza mdomoni mwake.
Baada ya kuweka moto huo mdomoni, moshi mkubwa ulionekana ukitoka ‘puani’ kwake jambo ambalo bado halijajulikana linawezekanaje na halijawahi kuonekana likitendeka.
Watafiti wa Jamii ya Uhifadhi wa Wanyamapori nchini India (WCS) ndio waliochukua video hiyo kipindi wanafanya maonesho ya tabia zisizo za kawaida za wanyamapori.
BREAKING: Wakurugenzi Wawili wasimamishwa kazi, baada ya Ripoti ya CAG