Katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa malaria barani Afrika, wanasayansi takriban elfu tatu wanakutana nchini Senegal kwa siku tano wiki hii katika mkutano wa saba wa kimataifa wa afya kujadili ugonjwa huo.
Shirika la Afya duniani (WHO) limeeleza kuwa linaamini nchi sita barani Afrika ambazo ni Algeria, Visiwa vya Comoro, Madagascar, Gambia, Zimbabwe na Senegal wana uwezo mkubwa wa kuutokomeza kabisa ugonjwa huo.
Inaelezwa kuwa watu 4,000,000 wanafariki kila mwaka kwa sababu ya ugonjwa wa malaria, wengi wao ikiwa ni watoto. Pia maambukizi ya ugonjwa huu yanatajwa kuongezeka katika nchi za Nigeria, Ivory Coast, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
‘Kwanini Zanzibar wamekuwa kati ya viwanja bora vya ndege, nyie hakuna’-Waziri Mbarawa