Azubuike Chibuzo Nelson ni msanii wa Hip Hop na producer pia kutoka Nigeria maarufu kwa jina la Phyno. Alianza muziki mwaka 2003 kama producer na mwaka 2012 aliachia album yake ya kwanza iitwayo No Guts No Glory ambayo ndani yake utapata ngoma kali zikiwemo Ghost Mode, Man of the Year, Parcel na O Set. Akiwa kama producer wa muziki ameshafanya kazi na wasanii kama Timaya, Flavour, Ruggedman, Bracket na J Martins wa Nigeria.
Phyno anajulikana sana kwa kazi zake za kimuziki na amekuwa ni mtu msiri sana kuhusiana na maisha yake binafsi, watu wengi hatuujui undani wa Phyno, mpenzi wake wala stori zozote za chini chini zinazomhusu yeye na wanawake… Lakini kwenye hii interview alioifanya Nigeria, swali kwa Phyno lilikuwa je anamzimia mwana dada Genevieve Nnaji ??
Hajalikwepa swali hilo, yapo majibu aliyoyatoa kujibu hilo.
>>> “Ninamkubali sana Genevieve na nahisi mimi ni shabiki wake namba mmoja … Genevieve ni staa wa Nigeria ninayemzimia yes, nahisi hiki sio kitu kibaya na inaruhusiwa kumzimia staa unayeikubali kazi yake katika industry ya entertainment, japo yeye amejikita sana kwenye uigizaji na biashara bado namzimia sana… Sioni tatizo na hata akijua bado hainizuii mimi kujisikia ninavyojisikia juu yake“>>> Phyno.
Alipoulizwa kama ana mpango wowote wa kumwambia Genevieve juu ya hisia zake na jinsi anvyomkubali msanii huyo, Phyno alizuga na kupotezea >>>“ Ahahaha bwana kausha, sina cha kusema!“>>>
Unahisi rapper Phyno ana mapenzi mengine anayomaanisha kwa Genevieve tofauti na upendo wako wa kuzikubali kazi zake za kisanii !?
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.