Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kifo cha aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mbunge wa Ushetu, Elias Kwandikwa kimeacha pengo Serikali na Bungeni kwani marehemu alikuwa mchapakazi, mwadilifu na mtulivu katika utendaji kazi wake.
Amesema hayo leo Jumatano (Agosti 4, 2021) alipokwenda nyumbani kwa marehemu Kwandikwa, Kibaha Picha ya Ndege mkoani Pwani kutoa pole kwa familia.
“Mchango wake wa utendaji katika Serikali na Bunge ni mkubwa sana alifanikiwa kuwavutia wengi kwa tabia yake ya upole, unyenyekevu na uzingatiaji wa taratibu na sheria za ik utumishi kila alipopangiwa kufanya kazi, hivyo kifo chake ni pigo kwa taifa”-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
SABABU YA KIFO CHA WAZIRI WA ULINZI TANZANIA “NI HOMA YA MAPAFU, UGUMU KATIKA UPUMUAJI”