Staa maarufu nchini Marekani, Amber Rose amewakutanisha baba wa watoto wake kwenye shughuli na kupiga nao picha ya pamoja iliyosambaa mtandaoni na kutengeneza headlines tofauti tofauti.
Kwenye picha hiyo aliyopost Amber kwenye ukurasa wake wa Instagram inamuonesha yupo na mpenzi wake wa sasa Alexander Edwards na Ex wake, rapa Wiz Khalifa wakiwa na watoto wao.
Kama utakumbuka Amber alifanikiwa kupata mtoto wake Sebastian Taylor akiwa kwenye uhusiano na rapa Wiz Khalifa huku Slash Electric alijifungua Oktoba mwaka jana akiwa mtoto wake wa pili, lakini ni mtoto wa kwanza na mpenzi wake wa sasa Alexander Edwards.