Ad

Top Stories

Picha za matukio mbalimbali Ikulu leo (+picha25)

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 06 Aprili, 2021 amewaapisha Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na wakuu wa taasisi aliowateua tarehe 04 Aprili, 2021.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Yustino Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Athman Kattanga, Mawaziri na Naibu Mawaziri, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, viongozi wa Dini na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Bw. Aboubakar Kunenge.

Soma na hizi

Tupia Comments