AyoTV

PICHA: Baada ya game ya Serengeti Boys vs Niger kumalizika

on

May 21 2017 Tanzania iliwania nafasi ya kuingia katika historia mpya ya soka la Afrika nchini Gabon kwa kucheza mchezo wake wa mwisho kwenye kundi B vs Niger katika michuano ya AFCON ya vijana wenye umri chini ya miaka 17.

Mpaka dakika 90 zinaisha, Serengeti Boys walikuwa wakihitaji sare au ushindi ili kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hii lakini kwa bahati mbaya game ikaisha Niger anaongoza 1-0 goli lililofungwa na Ibrahim kwenye dakika ya 42.

Tanzania licha ya kulingana kwa kila kitu na timu ya taifa ya Niger kwa wote kuwa na point sawa wanaondolewa katika michuano hii kwa kanuni ya wao kwa wao walipokutana nani alipoteza ndio maana Tanzania anaondolewa.

Niger na Mali wanafuzu nusu fainali ya michuano hii huku Angola na Tanzania zikiaga michuano hii.

VIDEO: Noma!! Mashindano ya magari Bagamoyo 2017…. tazama hii video hapa chini kujionea mwanzo mwisho

Soma na hizi

Tupia Comments